YANGA YATEMA WATATU SAFARI YA MAURITIUS




Jerry Muro-Afisa habari klabu ya Yanga
Jerry Muro-Afisa habari klabu ya Yanga
Kikosi cha Yanga SC kitaanza safari ya kuelekea Mauritius   kesho (Jumatano) alfajiri kwenda kukipiga mchezo wa awali wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Cercle De Joachim ya nchini humo.
Yanga itaondoka Dar kuelekea Mauritius ikiwa na kikosi cha wachezaji 21, viongozi wa 7 wa benchi la ufundi pamoja na mkuu wa msafara Ayoub Nyenzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
Wachezaji ambao hawato safari na timu ni Geofrey Mwashiuya, Benedict Tinoco ambao wanashughulikia passport ao za kusafiria pamoja na Matteo Anthony ambaye hayuko fit kimchezo.
Mchezo wa Yanga dhidi ya Cercle De Joachim umepangwa kuchezwa siku ya Jumamosi February 13 saa 9:30 alasiri kwa saa za Mauritius na utasimamiwa na waamuzi kutoka Madagascar wakati match commissioner anatoka  Msumbiji.
Kwa mujibu wa afisa habari wa Yanga Jerry Muro, mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Yanga hakita rejea moja kwa moja nchini bali kitaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuhezwa February 20 mwaka huu. SOMA ZAIDI

Comments

Popular posts from this blog

WANAOWANIA KUPANDA LIGI KUU BARA HAWA HAPA, KAZI IPO JUMAMOSI

AIBU!!! MIMBA YAMUUMBUA WEMA SEPETU

South Korea, U.S. begin exercises as North Korea threatens attack