WAWILI MBARONI KWA KUUZA TICKET FEKI SONGEA


Pingu
Hii ni soka series episodi ya nje ya uwanja,wakati mchezo kati ya Majimaji na Mgambo JKT kutoka Tanga unapigwa huku milangoni watu wakaona njia ya kupigia pesa duh!
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Katibu wa chama cha mpira wa miguu manispaa ya Songea (SUFA) mchezaji wa zamani wa vilabu kadhaa hapa nchini Kelvin  Haule na mkatisha tiketi Aron Mapunda kwa kosa la kuuza tiketi bandia katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ulopigwa juzi kati ya ‘Wanalizombe’ Majimaji FC dhidi ya  Mgambo JKT.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zubery Muhombeji naelezea mpango mzima ulivyokuwa katika sakata hilo linaloutia doa mpira wa Tanzania.
“Wakati wa majira wa saa 11 jioni wakati huo mpira tayari ulikuwa umeanza alikamatwa bwana mmoja ambaye alijulikana kwa jina la Aron Mapunda mkazi wa Majengo akiwa na ticketi 120 ambazo baadaye ziligundulika kwamba si halali zilikuwa ni ticket bandia”, amesema Muhombeji.
“Ticket hizo zimepatikana kwenye kitabu ambacho huwa kina ticketi 100 na baada ya uchunguzi ilikgundulika tayari alikuwa ameshauza ticketi 80 ambazo zilikuwa na thamani ya shilingi 157,000”.
“Ticket hizo zilionekana kwamba si halali kwani zilikuwa si rasmi kwa ajili ya mchezo wa Majimaji vs Mgambo JKT. Ticket hizo zilitumika katika mchezo uliopita ambao ulikuwa ni kati ya timu ya Majimaji vs Ndanda FC”.
“Lakini baada ya mahojiano Bw. Mapunda alimtaja bwana mmoja anaitwa Kelvin Haule kwamba ndiyr aliyempatia kitabu hicho cha ticket. Haule naye alikamatwa na wote wawili wamefikishwa kituo cha polisi kwa mahojiano, uchunguzi unakamilika ili baadaye waweze kufikishwa mahakamani”.
Ripota wetu hakuishia hapo akafunga safari hadi kwa Golden Sanga mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma FARU kutaka kujua kwanini madudu hayo yanatokea na kama kuna ukweli wowote kuhusu tiketi kumalizika na kama kuna ongezeko lolote la mapato kwenye ticket hizo bandia.
“Tulipohesabu fedha tumekuta kuna ongezeko la 157,000 ambazo ziko nje ya mauzo ya vitabu ambavyo vilikuwepo. Kwahiyo ni dhahiri kwamba zilikuwepo ticket ambazo zilikuwa zinauwa tofauti na zilikuwepo”, alisema Sanga.
“Majimaji ni timu yetu, waliohusika watu ambao tuko pamoja kwenye mpira. Jambo hili limekuwa likizungumzwa na kuelekezwa kwenye ofisi yangu na kwenye timu ya Majimaji yenyewe na leo limethibitika. Mimi ninaushahidi ninazo ticket za mchezo wa Majimaji vs Ndanda ambao ulichezwa mwaka jana zimeuzwa kwenye mchezo huu”.
“Ni vizuri hawa watu wachukuliwe hatua waende polisi wakajieleze ni kwa utaratibu gani. Kwasababu timu zote mbili zinatakiwa zikutane ticket zinapokuwa zimeisha na viongozi wa Faru wakutane nao wakubaliane kama kuna nyongeza ya ticket ifanywe kwa makubaliano. Jambo hilo halikufanyika”.

Comments

Popular posts from this blog

WANAOWANIA KUPANDA LIGI KUU BARA HAWA HAPA, KAZI IPO JUMAMOSI

AIBU!!! MIMBA YAMUUMBUA WEMA SEPETU

South Korea, U.S. begin exercises as North Korea threatens attack