KOCHA MBELGIJI ASEMA SAMATTA ATANG'ARA UBELGIJI LAKINI....
![]() |
| SAMATTA AKIWA KATIKA VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO VYA GENK |
Kocha
bora wa michuano ya Kombe la Chalenji msimu uliopita, Adel Amrouche
amesema mshambuliaji Mbwana Samatta ana nafasi ya kufanya vizuri akiwa
Ubelgiji.
Samatta
raia wa Tanzania, amejiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP
Mazembe, siku chache baada ya kutangazwa mchezaji bora wa Afrika.
![]() |
| AMROUCHE |
Amrouche
raia wa Ubelgiji, aliyipa Kenya ubingwa wa Chalenji huku ikiwa na
kikosi kinachoonekana hakina makali, amesema Samatta atafanya vizuri
kama ataendelea kujiamini, lakini aongeze juhudi.
“Lazima
aongeze juhudi, awe msikivu na asione tena kama yuko Afrika ambako
alikuwa staa. Sasa ndiyo anaanza upya,” alisema Amrouche mwenye asili ya
Algeria aliyewahi kuifundisha Motema Pembe ya Dr Congo.
Amrouche
ambaye anasifika kwa kuwainua makocha vijana, alisisitiza Samatta ana
kipaji na uwezo mkubwa. Lakini ushindani wa Ubelgiji unakuwa juu, lakini
ataweza kupambana.
Tayari nahodha huyo wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars amecheza dakika 17 akiwa na kikosi cha Genk


Comments
Post a Comment