WANAOWANIA KUPANDA LIGI KUU BARA HAWA HAPA, KAZI IPO JUMAMOSI
Wikiendi hii msimu wa Ligi Daraja la Kwanza 2015/16, unatarajiwa kuhitimishwa kwa kuchezwa mechi 12 katika viwanja tofauti huku timu zote 24 zikishuka dimbani, zipo zinazosaka pointi muhimu huku nyingine zikikamilisha ratiba tu kwani hazina cha kupoteza. Tayari Ruvu Shooting kutoka Kundi B, imeshajikatia tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao, huku JKT Kanembwa iliyokuwa Kundi C ikiwa ni timu ya kwanza kushuka daraja. Vita iliyobaki ni ya kutafuta nafasi ya kuungana na Ruvu Shooting na nyingine ni ile ya kuepuka kuifuata JKT Kanembwa. Katika vita ya kupanda, African Lyon inaongoza Kundi A ikiwa na pointi 26, inafuatiwa na Friends Rangers yenye pointi 23 sawa na Ashanti United inayoshika nafasi ya tatu, lakini tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ndiyo inayowatenganisha. Mechi zao za mwisho, African Lyon vs Ashanti na Friends vs Kiluvya United, hivyo basi endapo Friends ikiibuka na ushindi na Lyon ikapoteza basi Friends inapanda, lakini ...
Comments
Post a Comment